Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadéra, ameshinda muhula wa tatu katika uchaguzi uliofanywa mwezi uliopita. Muungano mkuu wa upinzani uliususia uchaguzi huo wa Desemba 28.